Matthew 4:18-22

18 aIsa alipokuwa anatembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake. Walikuwa wakizitupa nyavu zao baharini kwa kuwa wao walikuwa wavuvi. 19 bIsa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.” 20 cMara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

21 dAlipoendelea mbele kutoka pale, akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakizitengeneza nyavu zao. Isa akawaita. 22 eNao mara wakaiacha mashua yao, pamoja na baba yao, wakamfuata.

Isa Ahubiri Na Kuponya Wagonjwa

(Luka 6:17-19)

Copyright information for SwhKC